SIMULIZI FUPI, LOVE STORY
Kijana mmoja alitokea kumpenda sana dada mmoja ijapokuwa dada huyo alikuwa akimtolea nje mara kwa mara lakini kijana hakukata tamaa, akiendelea kurusha ndoano huku akiamini siku moja atafanikiwa.
Siku moja dada huyo akiwa yupo nyumbani aliamua kumpigia simu huyu kaka na kumtaka aje nyumbani kwake, yule kijana alifurahi na kuhisi sasa ombi lake limekubaliwa.
Akiwa nyumbani kwake dada huyo , alikuwa amevalia kanga moja laini, kutokana na hali ya hewa ya joto la Dar es salaam.Kwa upande wa yule kijana alikuwa amefurahi sana na haraka alijiandaa na kuanza safari kuelekea kwa huyu dada, njia ni kaka huyu alikuwa akijiuliza maswali mengi, huku akiwa haamini kama yule dada amemuita nyumbani kwake. Alipofika, alibisha hodi na yuel dada akafungua mlango huku akionyesha tabasamu pana katika paji la uso wake.
Kaka huyu aliingia ndani huku kijasho kikimteremka mithili ya mtu aliyekuwa anakimbia. Dada huyu alimkaribisha vizuri, yule kaka aliomba maji ya kunywa huku muda wote akimtizama kwa umakini dada huyu mrembo, aliyeumbika kila idara na ile kanga nyepesi aliyovaa ilikuwa ikionyesha umbo zuri la dada huyu ambaye waswahili huwa wanasema, mtoto kajaaliwa (mashalaah) Kaka alikuwa akivuta pumzi kwa haraka haraka, na kusema “Nimefurahi sana, umenikaribisha nyumbani kwako ni pazuri sana.”
Yule dada alitabasamu na kusema “Asante sana, nimefurahi pia umeitikia wito wangu, samahani kwa usumbufu wangu”.
Yule kaka alitabasamu huku akijisogeza sogeza “Hakuna tatizo, usijali kabisa, mimi nipo kwa ajili yako, naimani sasa nina….” Kabla hajamilizia kuongea yule dada alimshika mikono yake miwili huku akimtizama machoni, kwa macho yake malegevu, mithili ya mtu aliyekula kungu “Samahani kaka, mimi nimekuita hapa kuna jambo nataka unishauri, nataka kujua ni zawadi gani nzuri unaweza kumpatia mwanaume unayempenda”
Kaka yule alikuwa akitetemeka na kusema “Chochote tu, zawadi ni zawadi, alimradi kuwe na mapenzi ya kweli” Dada yule alitabasamu na kusema “Ni kweli, mapenzi ya kweli ndiyo jambo la msingi, nitampenda maisha yangu yote” Kaka yule akauliza “Utampenda? Nani huyo”
Yule dada alitabasamu tena na kusema “Samahani, rafiki nilikuwa sijakuambia, wiki ijayo nafunga ndoa na mpenzi wangu wa muda mrefu ambaye nampenda sana, na pia nilikuita ili nikupe kadi ya harusi, nitafurahi kukuona, kwani wewe ni rafiki yangu pia” Yule kaka alibaki amepigwa na butwaa, “Ati, nini unaolewa, daaah, jamani, kwahiyo.”
Alinyanyuka na kuondoka bila ya kuaga huku akimuacha yule dada anamuita ili ampatie kadi bila ya mafanikio.
SIYO KILA UNACHOKIWAZA MOYONI MWAKO KITATOKEA KAMA UNAVYOTAKA. KWAHIYO NI VYEMA KUJIANDAA KUKUBALIWA AU KUKATALIWA[/HEADING]
“Reshmail Manyama want to be your friend.’confirm’ ‘ignore’ ulikuwa ni ujumbe ambao macho yangu yalikutana nao nilipofungua mtandao wa kijamii wa ‘facebook’,sikumbuki kama nilijifikiria mara mbili kwani niliona ni jambo la kawaida sana kukutana na ‘notifications’ kama hizo,na mara zote neno confirm(kubali) lilipata fursa ya kutumika.
Hivyohivyo hata kwa Reshmail nilifanya hivyo.”You and reshmail are now friends” ndio ujumbe ulionisindikiza baada ya kukubali ombi lile kutoka kwa Reshmail.
Ni kijana mtanashati niliyebahatika kukutana nae pale chuo kikuu cha mtakatifu Augustine Mwanza,alijipenda kuanzia ndani ya chumba chake hadi mwili wake,ilikuwa ni nadra sana kumfumania akiwa amevaa nguo aliyoivaa jana, bila kumnyima haki yake nasema alikuwa anapendeza kila siku,macho yangu ya kipelelezi na kamera zangu za kipaparazi kamwe hazikufanikiwa kumjua aliyekuwa ubavu wa pili wa bwana huyu yaani ‘MPENZI’.
Ukipenda waweza kuniita kimbelembele lakini ukiniita hivyo basi majina hayo yatakuwa mengi pale chuoni kwani wengi walikuwa na shauku kubwa ya kujua siri hiyo na kamwe hawakufanikiwa.
Binadamu hatuna dogo watu washaanza kusema eti huenda jamaa ana matatizo makubwa tu mwilini mwake ndio maana yuko peke yake licha ya kushobokewa na wasichana warembo, mh! mimi sikuwa mmoja wao lakin nilijiuliza pia kulikoni?
Makala mbovu zilizokuwa zinaandikwa na gazeti la chuo lililojulikana kama ‘Saut voice’ ndo zilinizonivuta zaidi kutaka na mimi siku moja kuandika katika gazeti hilo lililokosa mvuto siku za hivi karibuni makala nzuri itakayorudisha heshima ya gazeti hilo.
Taratibu nilijenga mazoea na hatimaye nikafanikiwa kumzoea “THE MOST WANTED” ucheshi wangu ndio uliomvutia zaidi kupenda kuwa karibu nami pamoja na mchezo wa mpira wa miguu kwani wote tulikuwa mashabiki wakubwa,haukupita mwezi mzima nikawa nina uwezo wa kuanza kazi yangu, ni mimi na Adam Michael kwenye meza moja chumban kwangu ananipa hadithi yake ya maisha yaliyomfanya awe kama alivyo.
“Aah!! jamani Reshmail…” alianza Adam,yangu masikio na macho nikaanza kusikiliza kwa makini.
Comment zenu ndizo zitaamua story iendelee au